Yer. 25:23-34 Swahili Union Version (SUV)

23. Dedani, na Tema, na Buzi, na watu wote wakatao denge;

24. na wafalme wote wa Arabuni, na wafalme wote wa watu waliochanganyika wakaao jangwani;

25. na wafalme wote wa Zimri, na wafalme wote wa Elamu, na wafalme wote wa Wamedi;

26. na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na wafalme wote wa dunia, wakaao juu ya uso wa dunia; na mfalme wa Sheshaki atakunywa baada yao.

27. Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu.

28. Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa.

29. Maana angalieni, ninaanza kutenda mabaya katika mji uitwao kwa jina langu, je! Mtaachiliwa ninyi msiadhibiwe? Hamtaachiliwa msiadhibiwe; kwa maana nitauita upanga ule uwapige wote wakaao katika dunia, asema BWANA wa majeshi.

30. Basi, tabiri wewe maneno haya yote juu yao, na kuwaambia,BWANA atanguruma toka juu,Naye atatoa sauti yake toka patakatifu pake;Atanguruma sana juu ya zizi lake;Atapiga kelele kama mtu akanyagaye zabibu,Juu ya wenyeji wote wa dunia.

31. Mshindo utafika hata mwisho wa dunia;Maana BWANA ana mashindano na mataifa,Atateta na watu wote wenye mwili;Na waovu atawatoa wauawe kwa upanga; asema BWANA.

32. BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.

33. Na waliouawa na BWANA siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi.

34. Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.

Yer. 25