Wim. 8:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Laiti ungekuwa kama ndugu yangu,Aliyeyanyonya matiti ya mamangu!Kama ningekukuta huko nje,Ningekubusu, asinidharau mtu.

2. Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu,Naye angenifundisha;Ningekunywesha divai iliyokolea,Divai mpya ya mkomamanga wangu.

3. Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu,Nao wa kuume ungenikumbatia.

4. Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwani kuyachochea mapenzi, au kuyaamsha,Hata yatakapoona vema?

5. Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,Akimtegemea mpendwa wake?Nalikuamsha chini ya huo mpera;Huko mama yako alikuonea utungu,Aliona utungu aliyekuzaa.

6. Nitie kama muhuri moyoni mwako,Kama muhuri juu ya mkono wako;Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,Na wivu ni mkali kama ahera.Mwako wake ni mwako wa moto,Na miali yake ni miali ya Yahu.

7. Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,Wala mito haiwezi kuuzamisha;Kama mtu angetoa badala ya upendoMali yote ya nyumbani mwake,Angedharauliwa kabisa.

Wim. 8