Nitie kama muhuri moyoni mwako,Kama muhuri juu ya mkono wako;Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,Na wivu ni mkali kama ahera.Mwako wake ni mwako wa moto,Na miali yake ni miali ya Yahu.