7. Walinzi wazungukao mjini waliniona,Wakanipiga na kunitia jeraha,Walinzi walindao kuta zakeWakaninyang’anya shela yangu.
8. Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Ninyi mkimwona mpendwa wangu,Ni nini mtakayomwambia?Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.
9. Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako,Wewe uliye mzuri katika wanawake,Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako,Hata wewe utusihi hivyo?
10. Mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu,Mashuhuri miongoni mwa elfu kumi;
11. Kichwa chake ni kama dhahabu safi sana,Nywele zake ni za ukoka, nyeusi kama kunguru;
12. Macho yake ni kama hua penye vijito,Wakioga kwa maziwa, wakiikalia mito iliyojaa;
13. Mashavu yake ni kama matuta ya rihani,Ambayo hufanyizwa manukato;Midomo yake ni kama nyinyoro,Inadondoza matone ya manemane;
14. Mikono yake ni kama mianzi ya dhahabu,lliyopambwa kwa zabarajadi;Kiwiliwili chake kama kazi ya pembe,Iliyonakishiwa kwa yakuti samawi;
15. Miguu yake ni kama nguzo za marimari,Zilizowekwa juu ya misingi ya dhahabu;Sura yake ni kama Lebanoni,Ni bora mfano wa mierezi;