Wim. 3:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu,Nalimtafuta, nisimpate.

2. Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini,Katika njia zake na viwanjani,Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu.Nikamtafuta, nisimpate.

3. Walinzi wazungukao mjini waliniona;Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?

4. Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea,Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu;Nikamshika, nisimwache tena,Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu,Chumbani mwake aliyenizaa.

5. Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwa paa na kwa ayala wa porini,Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,Hata yatakapoona vema yenyewe.

6. Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,Mfano wake ni nguzo za moshi;Afukizwa manemane na ubani,Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?

7. Tazama, ni machela yake Sulemani;Mashujaa sitini waizunguka,Wa mashujaa wa Israeli.

Wim. 3