Malango yake yamezama katika nchi;Ameyaharibu makomeo yake na kuyavunja;Mfalme wake na wakuu wake wanakaaKati ya mataifa wasio na sheria;Naam, manabii wake hawapati maonoYatokayo kwa BWANA.