9. Yuda ni mwana-simba,Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda;Aliinama akajilaza kama simba,Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?
10. Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda,Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii.
11. Atafunga punda wake katika mzabibu,Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri.Amefua nguo zake kwa mvinyo,Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
12. Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo,Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
13. Zabuloni atakaa pwani ya bahari,Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu,Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
14. Isakari ni punda hodari,Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;
15. Akaona mahali pa raha, kuwa pema,Na nchi, ya kuwa ni nzuri,Akainama bega lake lichukue mizigo,Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.
16. Dani atahukumu watu wake,Kama moja ya makabila ya Israeli;
17. Dani atakuwa nyoka barabarani,Bafe katika njia,Aumaye visigino vya farasi,Hata apandaye ataanguka chali.
18. Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.
19. Gadi, jeshi litamsonga,Lakini atawasonga wao mpaka visigino.
20. Asheri, chakula chake kitakuwa kinono,Naye atatoa tunu za kifalme.
21. Naftali ni ayala aliyefunguliwa;Anatoa maneno mazuri.
22. Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa,Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi,Matwi yake yametanda ukutani.