1. Tupa chakula chako usoni pa maji;Maana utakiona baada ya siku nyingi.
2. Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane;Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi.
3. Mawingu yakiwa yamejaa mvua,Yataimimina juu ya nchi;Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini,Paangukapo ule mti, papo hapo utalala.
4. Mwenye kuuangalia upepo hatapanda;Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.
5. Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.