29. Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo.
30. Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?
31. Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.
32. Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili,Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo,Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya,Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
33. Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa.Ni nani atakayeeleza kizazi chake?Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.
34. Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?
35. Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.
36. Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? [