Kum. 33:10-16 Swahili Union Version (SUV)

10. Watamfundisha Yakobo hukumu zako,Na Israeli torati yako,Wataweka uvumba mbele zako,Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako.

11. Ee BWANA, ubariki mali zake,Utakabali kazi ya mikono yake;Uwapige viuno vyao waondokao juu yake,Na wenye kumchukia, wasiinuke tena.

12. Akamnena Benyamini,Mpenzi wa BWANA atakaa salama kwake;Yuamfunika mchana kutwa,Naye hukaa kati ya mabega yake.

13. Na Yusufu akamnena,Nchi yake na ibarikiwe na BWANA;Kwa vitu vya thamani vya mbinguni, kwa huo umande,Na kwa kilindi kilalacho chini,

14. Na kwa vitu vilivyo bora vya matunda ya jua,Na kwa vitu vilivyo bora vya maongeo ya miezi,

15. Na kwa vitu viteule vya milima ya kale,Na kwa vitu vilivyo bora vya vilima vya milele,

16. Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake,Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kijiti;Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu,Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze.

Kum. 33