8. Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao,Alipowabagua wanadamu,Aliweka mipaka ya watuKwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.
9. Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake,Yakobo ni kura ya urithi wake.
10. Alimkuta katika nchi ya ukame,Na katika jangwa tupu litishalo;Alimzunguka, akamtunza;Akamhifadhi kama mboni ya jicho;
11. Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake;Na kupapatika juu ya makinda yake,Alikunjua mbawa zake, akawatwaa,Akawachukua juu ya mbawa zake;
12. BWANA peke yake alimwongoza,Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye.
13. Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka,Naye akala mazao ya mashamba;Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini,Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;
14. Siagi ya ng’ombe, na maziwa ya kondoo,Pamoja na mafuta ya wana-kondoo,Kondoo waume wa Kibashani, na mbuzi,Na unono wa ngano iliyo nzuri;Ukanywa divai, damu ya mizabibu.
15. Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke;Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda;Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya,Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
16. Wakamtia wivu kwa miungu migeni,Wakamkasirisha kwa machukizo.