29. Laiti wangekuwa na akili, hata wakafahamu haya,Ili watafakari mwisho wao.
30. Mmoja angefukuzaje watu elfu,Wawili wangekimbizaje elfu kumi,Kama Mwamba wao asingaliwauza,Kama BWANA asingaliwatoa?
31. Maana, Mwamba wao si kama Mwamba wetu,Hata adui zetu wenyewe ndivyo wahukumuvyo.
32. Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma,Nao ni wa mashamba ya Gomora;Zabibu zao ni zabibu za uchungu,Vichala vyao ni vichungu.
33. Mvinyo yao ni sumu ya majoka,Uchungu mkali wa nyoka.
34. Je! Haya hayakuwekwa akiba kwangu?Na kutiwa muhuri kati ya hazina yangu?
35. Kisasi ni changu mimi, na kulipa,Wakati itakapoteleza miguu yao;Maana siku ya msiba wao imekaribia,Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.
36. Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake,Atawahurumia watumwa wake,Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka,Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa,
37. Naye atasema, Iko wapi miungu yao,Mwamba ule walioutumaini;
38. Uliokula shahamu za sadaka zao,Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji?Na waondoke na kuwasaidia ninyi;Na wawe hao himaya yenu.
39. Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye,Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi;Naua Mimi, nahuisha Mimi,Nimejeruhi, tena naponya;Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,
40. Maana, nainua mkono wangu mbinguni,Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele,