Kum. 32:16-23 Swahili Union Version (SUV)

16. Wakamtia wivu kwa miungu migeni,Wakamkasirisha kwa machukizo.

17. Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu,Kwa miungu wasiyoijua,Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu,Ambayo baba zenu hawakuiogopa.

18. Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa,Mungu aliyekuzaa umemsahau.

19. BWANA akaona, akawachukia,Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake.

20. Akasema, Nitawaficha uso wangu,Nitaona mwisho wao utakuwaje;Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi,Watoto wasio imani ndani yao.

21. Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu;Wamenikasirisha kwa ubatili wao;Nami nitawatia wivu kwa wasio watu,Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.

22. Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu,Unateketea hata chini ya kuzimu,Unakula dunia pamoja na mazao yake,Unaunguza misingi ya milima.

23. Nitaweka madhara juu yao chunguchungu;Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe;

Kum. 32