Isa. 25:8-12 Swahili Union Version (SUV)

8. Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.

9. Katika siku hiyo watasema,Tazama, huyu ndiye Mungu wetu,Ndiye tuliyemngoja atusaidie;Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja,Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.

10. Kwa maana mkono wa BWANA utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji ya jaa.

11. Naye atanyosha mikono yake katikati yake, kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono yake ili aogelee, naye atashusha kiburi chake, pamoja na hila za mikono yake.

12. Na boma la ngome ya kuta zako ameliinamisha, na kulilaza chini, na kulitupa chini hata mavumbini.

Isa. 25