Isa. 12 Swahili Union Version (SUV)

Shukrani na Sifa

1. Na katika siku hiyo utasema,Ee BWANA, nitakushukuru wewe;Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia,Hasira yako imegeukia mbali,Nawe unanifariji moyo.

2. Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;Nitatumaini wala sitaogopa;Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu;Naye amekuwa wokovu wangu.

3. Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.

4. Na katika siku hiyo mtasema,Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake;Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,Litajeni jina lake kuwa limetukuka.

5. Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu;Na yajulikane haya katika dunia yote.

6. Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.