1. Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza BWANA kuwabariki Israeli, hakwenda, kama hapo kwanza, ili kutafuta uchawi, bali alielekeza uso wake jangwani.
2. Balaamu akainua macho yake akawaona Israeli wamekaa kabila kabila; roho ya Mungu ikamjia.
3. Akatunga mithali yake, akasema,Balaamu mwana wa Beori asema,Yule mtu aliyefumbwa macho asema;
4. Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu,Yeye aonaye maono ya Mwenyezi,Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho;
5. Mahema yako ni mazuri namna gani, Ee Yakobo,Maskani zako, Ee Israeli!
6. Mfano wa bonde zimetandwa,Mfano wa bustani kando ya mto,Mfano wa mishubiri aliyoipanda BWANA,Mfano wa mierezi kando ya maji.
7. Maji yatafurika katika ndoo zake,Na mbegu zake zitakuwa katika maji mengi.Na mfalme wake ataadhimishwa kuliko Agagi,Na ufalme wake utatukuzwa.