8. Walichagua miungu mipya,Ndipo kulikuwa na vita malangoni;Je! Ilionekana ngao au mkukiKatika watu elfu arobaini wa Israeli?
9. Moyo wangu unawaelekea maliwali wa Israeli,Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu;Mhimidini BWANA.
10. Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe,Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani,Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu.
11. Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji,Hapo watatangaza matendo ya haki ya BWANA;Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli.Ndipo watu wa BWANA waliposhuka malangoni.
12. Amka, amka, Debora;Amka, amka, imba wimbo.Inuka, Baraka, wachukue mateka waoWaliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu.
13. Ndipo walitelemka mabaki ya waungwana na ya watu;BWANA alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa.