16. Mbona ulikaa katika mazizi ya kondoo,Kusikiliza filimbi zipigwazo ili kuita makundi?Kwenye vijito vya ReubeniPalikuwa na makusudi makuu mioyoni.
17. Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani,Na Dani, mbona alikaa katika merikebu?Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari,Alikaa katika hori zake.
18. Zabuloni ndio watu waliohatirisha roho zao hata kufa;Nao Naftali mahali palipoinuka kondeni.
19. Wafalme walikuja wakafanya vita,Ndipo wafalme wa Kanaani walifanya vita.Katika Taanaki, karibu na maji ya Megido;Hawakupata faida yo yote ya fedha.
20. Walipigana kutoka mbinguni,Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.
21. Mto ule wa Kishoni uliwachukua,Ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.Ee roho yangu, endelea mbele kwa nguvu.
22. Ndipo kwato za farasi zilikanyaga-kanyagaKwa sababu ya kupara-para,Kupara-para kwao wenye nguvu.
23. Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA,Walaanini kwa uchungu wenyeji wake;Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA,Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.