8. Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi, mwana wa Sauli, adui yako, aliyekutafuta roho yako; BWANA amemlipia kisasi bwana wangu mfalme hivi leo, juu ya Sauli, na juu ya wazao wake.
9. Naye Daudi akawajibu Rekabu na Baana, nduguye, wana wa Rimoni, Mbeerothi, akawaambia, Aishivyo BWANA, aliyenihifadhi roho yangu katika shida zote,
10. mtu mmoja aliponiambia, akasema, Tazama, Sauli amekufa, akidhani ya kuwa ameleta habari njema, nalimshika, nikamwua, huko Siklagi, ndio ujira niliompa kwa habari zake.
11. Basi, iwapo watu waovu wamemwua mtu mwenye haki kitandani mwake, je! Sasa nisitake zaidi damu yake mikononi mwenu, na kuwaondoa ninyi katika nchi?