Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi, mwana wa Sauli, adui yako, aliyekutafuta roho yako; BWANA amemlipia kisasi bwana wangu mfalme hivi leo, juu ya Sauli, na juu ya wazao wake.