1. Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi.Daudi, mwana wa Yese, anena,Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu,Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo,Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;
2. Roho ya BWANA ilinena ndani yangu,Na neno lake likawa ulimini mwangu.
3. Mungu wa Israeli alisema,Mwamba wa Israeli aliniambia,Atawalaye wanadamu kwa haki,Akitawala katika kicho cha Mungu,
4. Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo,Asubuhi isiyo na mawingu.Lachipuza majani mabichi juu ya nchi,Kwa mwangaza baada ya mvua;
5. Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA?Kwa kuwa amefanya nami agano la milele;Ina taratibu katika yote, ni thabiti,Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.
6. Lakini hatawachipuza watu wa ubatili;Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa,Ambayo haivuniki kwa mkono,
7. Mtu atakayeigusa hiyo,Na awe na chuma na mpini wa mkuki,Nao watateketezwa papo hapo kwa moto.
8. Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni, mkuu wa maakida; huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja.
9. Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;
10. huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye BWANA akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu.