2 Sam. 1:15-27 Swahili Union Version (SUV)

15. Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa.

16. Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa BWANA.

17. Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya;

18. (kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari), akasema,Wana wa Yuda na wafundishwe haya,

19. Walio fahari yako, Ee IsraeliJuu ya mahali pako palipoinuka wameuawa;Jinsi mashujaa walivyoanguka!

20. Msiyahubiri mambo haya katika Gathi,Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni;Wasije wakashangilia binti za Wafilisti,Binti za wasiotahiriwa wakasimanga.

21. Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenuUmande wala mvua, wala mashamba ya matoleo;Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa,Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.

22. Kutoka kwa damu yao waliouawa,Kutoka kwa shahamu yao mashujaa,Upinde wa Yonathani haukurudi nyuma,Wala upanga wa Sauli haukurudi bure.

23. Sauli na Yonathani walipendwa na kupendezaMaishani wala mautini hawakutengwa;Walikuwa wepesi kuliko tai,Walikuwa hodari kuliko simba.

24. Enyi binti za Israeli, mlilieniHuyo Sauli, ambaye aliwavikaMavazi mekundu kwa anasa,Akazipamba nguo zenu dhahabu.

25. Jinsi mashujaa walivyoangukaKatikati ya vita!Ee Yonathani, wewe umeuawaJuu ya mahali pako palipoinuka

26. Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu,Ulikuwa ukinipendeza sana;Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu,Kupita upendo wa wanawake.

27. Jinsi mashujaa walivyoanguka,Na silaha za vita zilivyoangamia!

2 Sam. 1