2 Nya. 4:9-19 Swahili Union Version (SUV)

9. Tena akaufanya ua wa makuhani, na ua mkubwa, nayo milango yake, akaifunikiza kwa shaba milango yake.

10. Nayo bahari akaiweka upande wa kuume kwa mashariki, kuelekea kusini.

11. Na Huramu akayafanya masufuria, na majembe, na mabakuli.Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu;

12. zile nguzo mbili, na vimbe, na taji mbili zilizokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuzifunika vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo;

13. na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuzifunika vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo.

14. Akayafanya na matako, na mabirika akafanya juu ya matako;

15. bahari moja, na ng’ombe kumi na wawili chini yake.

16. Masufuria pia, na majembe, na nyuma, na vyombo vyake vyote, Huramu akamfanyia mfalme Sulemani kwa nyumba ya BWANA, vya shaba iliyokatuka.

17. Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda.

18. Ndivyo alivyovifanya Sulemani vyombo hivyo vyote, vingi sana; kwa kuwa uzani wa shaba ulikuwa hautafutikani.

19. Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho;

2 Nya. 4