Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya BWANA. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu.