2 Nya. 27:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; na jina la mamaye aliitwa Yerusha binti Sadoki.

2. Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, sawasawa na yote aliyoyafanya Uzia babaye; isipokuwa hakuingia hekaluni mwa BWANA. Lakini watu walikuwa wakali kufanya maovu.

3. Ndiye aliyelijenga lango la juu la nyumba ya BWANA, na juu ya ukuta wa Ofeli akajenga sana.

4. Tena akajenga miji katika milima ya Yuda, na mwituni akajenga ngome na minara.

2 Nya. 27