Zab. 97:7-11 Swahili Union Version (SUV)

7. Na waaibishwe wote waabuduo sanamu,Wajivunao kwa vitu visivyofaa;Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.

8. Sayuni imesikia na kufurahi,Binti za Yuda walishangilia,Kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA.

9. Maana Wewe, BWANA, ndiwe Uliye juu,Juu sana kuliko nchi yote;Umetukuka sana juu ya miungu yote.

10. Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu;Huwalinda nafsi zao watauwa wake,Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.

11. Nuru imemzukia mwenye haki,Na furaha wanyofu wa moyo.

Zab. 97