Zab. 97:5-10 Swahili Union Version (SUV)

5. Milima iliyeyuka kama nta mbele za BWANA,Mbele za Bwana wa dunia yote.

6. Mbingu zimetangaza haki yake,Na watu wote wameuona utukufu wake.

7. Na waaibishwe wote waabuduo sanamu,Wajivunao kwa vitu visivyofaa;Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.

8. Sayuni imesikia na kufurahi,Binti za Yuda walishangilia,Kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA.

9. Maana Wewe, BWANA, ndiwe Uliye juu,Juu sana kuliko nchi yote;Umetukuka sana juu ya miungu yote.

10. Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu;Huwalinda nafsi zao watauwa wake,Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.

Zab. 97