Zab. 79:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako,Wamelinajisi hekalu lako takatifu.Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.

2. Wameziacha maiti za watumishi wakoZiwe chakula cha ndege wa angani.Na miili ya watauwa wakoIwe chakula cha wanyama wa nchi.

3. Wamemwaga damu yao kama majiPande zote za Yerusalemu,Wala hapakuwa na mzishi.

4. Tumekuwa lawama kwa jirani zetu,Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.

5. Ee BWANA, hata lini? Utaona hasira milele?Wivu wako utawaka kama moto?

6. Ukali wako uwamwagie mataifa wasiokujua,Na falme za hao wasioliitia jina lako.

Zab. 79