Zab. 78:5-19 Swahili Union Version (SUV)

5. Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo,Na sheria aliiweka katika Israeli.Aliyowaamuru baba zetuWawajulishe wana wao,

6. Ili kizazi kingine wawe na habari,Ndio hao wana watakaozaliwa.Wasimame na kuwaambia wana wao

7. Wamwekee Mungu tumaini lao.Wala wasiyasahau matendo ya Mungu,Bali wazishike amri zake.

8. Naam, wasiwe kama baba zao,Kizazi cha ukaidi na uasi.Kizazi kisichojitengeneza moyo,Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.

9. Wale Waefraimu, wenye silaha, wapiga upinde,Walirudi nyuma siku ya vita.

10. Hawakulishika agano la Mungu;Wakakataa kuenenda katika sheria yake;

11. Wakayasahau matendo yake,Na mambo yake ya ajabu aliyowaonyesha.

12. Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu,Katika nchi ya Misri, konde la Soani.

13. Aliipasua bahari akawavusha;Aliyasimamisha maji mfano wa chungu.

14. Akawaongoza kwa wingu mchana,Na usiku kucha kwa nuru ya moto.

15. Akapasua miamba jangwani;Akawanywesha maji mengi kama maji ya vilindi.

16. Akatokeza na vijito gengeni,Akatelemsha maji kama mito.

17. Lakini wakazidi kumtenda dhambi,Walipomwasi Aliye juu katika nchi ya kiu.

18. Wakamjaribu Mungu mioyoni mwaoKwa kutaka chakula kwa tamaa zao.

19. Naam, walimwamba Mungu, wakasema,Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?

Zab. 78