1. Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu,Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu.
2. Na nifunue kinywa changu kwa mithali,Niyatamke mafumbo ya kale.
3. Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu,Ambayo baba zetu walituambia.
4. Hayo hatutawaficha wana wao,Huku tukiwaambia kizazi kingine,Sifa za BWANA, na nguvu zake,Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya.