Zab. 7:7-16 Swahili Union Version (SUV)

7. Kusanyiko la mataifa na likuzunguke,Na juu yake uketi utawale.

8. BWANA atawaamua mataifa,BWANA, unihukumu mimi,Kwa kadiri ya haki yangu,Sawasawa na unyofu nilio nao.

9. Ubaya wao wasio haki na ukome,Lakini umthibitishe mwenye haki.Kwa maana mjaribu mioyo na viunoNdiye Mungu aliye mwenye haki.

10. Ngao yangu ina Mungu,Awaokoaye wanyofu wa moyo.

11. Mungu ni mwamuzi mwenye haki,Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku.

12. Mtu asiporejea ataunoa upanga wake;Ameupinda uta wake na kuuweka tayari;

13. Naye amemtengenezea silaha za kufisha,Akifanya mishale yake kuwa ya moto.

14. Tazama, huyu ana utungu wa uovu,Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.

15. Amechimba shimo, amelichimba chini sana,Akatumbukia katika handaki aliyoifanya!

16. Madhara yake yatamrejea kichwani pake,Na dhuluma yake itamshukia utosini.

Zab. 7