6. Milima waiweka imara kwa nguvu zako,Huku ukijifunga uweza kama mshipi.
7. Wautuliza uvumi wa bahari,Uvumi wa mawimbi yake,Na ghasia ya mataifa;
8. Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako;Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
9. Umeijilia nchi na kuisitawisha,Umeitajirisha sana;Mto wa Mungu umejaa maji;Wawaruzuku watu nafakaMaana ndiwe uitengenezaye ardhi.
10. Matuta yake wayajaza maji;Wapasawazisha palipoinuka,Wailainisha nchi kwa manyunyu;Waibariki mimea yake.
11. Umeuvika mwaka taji ya wema wako;Mapito yako yadondoza unono.
12. Huyadondokea malisho ya nyikani,Na vilima vyajifunga furaha.