3. Hata lini mtamshambulia mtu,Mpate kumwua ninyi nyote pamoja?Kama ukuta unaoinama,Kama kitalu kilicho tayari kuanguka,
4. Hufanya shauri kumwangusha tu katika cheo chake;Huufurahia uongo.Kwa kinywa chao hubariki;Kwa moyo wao hulaani.
5. Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya.Tumaini langu hutoka kwake.
6. Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,Ngome yangu, sitatikisika sana.
7. Kwa Mungu wokovu wangu,Na utukufu wangu;Mwamba wa nguvu zangu,Na kimbilio langu ni kwa Mungu.
8. Enyi watu, mtumainini sikuzote,Ifunueni mioyo yenu mbele zake;Mungu ndiye kimbilio letu.