Zab. 6:5-9 Swahili Union Version (SUV)

5. Maana mautini hapana kumbukumbu lako;Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?

6. Nimechoka kwa kuugua kwangu;Kila usiku nakieleza kitanda changu;Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu.

7. Jicho langu limeharibika kwa masumbufu,Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.

8. Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu;Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.

9. BWANA ameisikia dua yangu;BWANA atayatakabali maombi yangu.

Zab. 6