1. BWANA, usinikemee kwa hasira yako,Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.
2. BWANA, unifadhili, maana ninanyauka;BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.
3. Na nafsi yangu imefadhaika sana;Na Wewe, BWANA, hata lini?
4. BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu,Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
5. Maana mautini hapana kumbukumbu lako;Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?