1. Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi,Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe.Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako,Hata misiba hii itakapopita.
2. Nitamwita MUNGU Aliye juu,Mungu anitimiziaye mambo yangu.
3. Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa,Atukanapo yule atakaye kunimeza.Mungu atazipelekaFadhili zake na kweli yake
4. Nafsi yangu i kati ya simba,Nitastarehe kati yao waliowaka moto.Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale,Na ndimi zao ni upanga mkali.
5. Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.