Zab. 45:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Moyo wangu umefurika kwa neno jema,Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme;Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.

2. Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu;Neema imemiminiwa midomoni mwako,Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.

3. Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari,Utukufu ni wako na fahari ni yako.

4. Katika fahari yako usitawi uendeleeKwa ajili ya kweli na upole na hakiNa mkono wako wa kuumeUtakufundisha mambo ya kutisha.

5. Mishale yako ni mikali, watu huanguka chini yako;Imo mioyoni mwa adui za mfalme.

6. Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele,Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

7. Umeipenda haki;Umeichukia dhuluma.Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta,Mafuta ya furaha kuliko wenzako.

8. Mavazi yako yote hunukia manemaneNa udi na mdalasini.Katika majumba ya pembeVinubi vimekufurahisha.

Zab. 45