Zab. 44:2-11 Swahili Union Version (SUV)

2. Wewe kwa mkono wako uliwafukuza mataifa,Ukawakalisha wao.Wewe uliwatesa watu wa nchi,Ukawaeneza wao.

3. Maana si kwa upanga wao walivyoimiliki nchi,Wala si mkono wao uliowaokoa;Bali mkono wako wa kuume, naam, mkono wako,Na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwaridhia.

4. Ee Mungu, Wewe ndiwe mfalme wangu,Uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo.

5. Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu;Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao.

6. Maana sitautumainia upinde wangu,Wala upanga wangu hautaniokoa.

7. Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu;Na watuchukiao umewaaibisha.

8. Tumejisifia Mungu mchana kutwa,Na jina lako tutalishukuru milele.

9. Lakini umetutupa, umetufedhehesha,Wala hutoki na majeshi yetu.

10. Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo,Na watuchukiao wanajipatia mateka.

11. Umetutoa kama kondoo tuwe chakula,Na kututawanya kati ya mataifa.

Zab. 44