8. Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami,Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.
9. Nitamwambia Mungu, mwamba wangu, Kwa nini umenisahau?Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
10. Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu,Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?