1. Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji.Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
2. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai,Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
3. Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku,Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako.
4. Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu,Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano,Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu,Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
5. Nafsi yangu, kwa nini kuinama,Na kufadhaika ndani yangu?Umtumaini Mungu;Kwa maana nitakuja kumsifu,Aliye afya ya uso wangu,Na Mungu wangu.
6. Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka,Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari.