13. Ee BWANA, uwe radhi kuniokoa,Ee BWANA, unisaidie hima.
14. Waaibike, wafedheheke pamoja,Wanaoitafuta nafsi yangu waiangamize.Warudishwe nyuma, watahayarishwe,Wapendezwao na shari yangu.
15. Wakae hali ya ukiwa, na iwe aibu yao,Wanaoniambia, Ewe! Ewe!
16. Washangilie, wakufurahie,Wote wakutafutao.Waupendao wokovu wakoWaseme daima, Atukuzwe BWANA.