Zab. 35:16-27 Swahili Union Version (SUV)

16. Kama wenye mzaha wakikufuru karamuniWananisagia meno.

17. BWANA, hata lini utatazama?Uiokoe nafsi yangu na maharabu yao,Na mpenzi wangu na wana-simba.

18. Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa;Nitakusifu kati ya watu wengi.

19. Walio adui zangu bure wasinisimange,Wanaonichukia bila sababu wasining’ong’e.

20. Maana hawasemi maneno ya amani,Na juu ya watulivu wa nchi huwaza hila.

21. Nao wananifumbulia vinywa vyao,Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona.

22. Wewe, BWANA, umeona, usinyamaze;Ee Bwana, usiwe mbali nami.

23. Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumuKwa ajili ya madai yangu,Mungu wangu na Bwana wangu.

24. Unihukumu kwa haki yako,Ee BWANA, Mungu wangu,Wala wasinisimangize.

25. Wasiseme moyoni, Haya! Ndivyo tutakavyo;Wasiseme, Tumemmeza.

26. Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja,Wanaoifurahia hali yangu mbaya.Wavikwe aibu na fedheha,Wanaojikuza juu yangu.

27. Washangilie na kufurahi,Wapendezwao na haki yangu.Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA,Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.

Zab. 35