10. Mifupa yangu yote itasema,BWANA, ni nani aliye kama Wewe?Umponyaye maskini na mtu aliye hodari kumshinda yeye,Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
11. Mashahidi wa udhalimu wanasimama,Wananiuliza mambo nisiyoyajua.
12. Wananilipa mabaya badala ya mema,Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa.
13. Bali mimi, walipougua wao,Nguo yangu ilikuwa gunia.Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga;Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.
14. Nalijifanya kama kwamba ni rafiki au ndugu yangu,Naliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.
15. Lakini nikijikwaa hufurahi na kukusanyana,Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua,Wananipapura wala hawakomi.
16. Kama wenye mzaha wakikufuru karamuniWananisagia meno.
17. BWANA, hata lini utatazama?Uiokoe nafsi yangu na maharabu yao,Na mpenzi wangu na wana-simba.
18. Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa;Nitakusifu kati ya watu wengi.
19. Walio adui zangu bure wasinisimange,Wanaonichukia bila sababu wasining’ong’e.
20. Maana hawasemi maneno ya amani,Na juu ya watulivu wa nchi huwaza hila.
21. Nao wananifumbulia vinywa vyao,Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona.