Zab. 25:18-21 Swahili Union Version (SUV)

18. Utazame teso langu na taabu yangu;Unisamehe dhambi zangu zote.

19. Uwatazame adui zangu, maana ni wengi,Wananichukia kwa machukio ya ukali.

20. Unilinde nafsi yangu na kuniponya,Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe.

21. Ukamilifu na unyofu zinihifadhi,Maana nakungoja Wewe.

Zab. 25