16. Uniangalie na kunifadhili,Maana mimi ni mkiwa na mteswa.
17. Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi,Na kunitoa katika dhiki zangu.
18. Utazame teso langu na taabu yangu;Unisamehe dhambi zangu zote.
19. Uwatazame adui zangu, maana ni wengi,Wananichukia kwa machukio ya ukali.
20. Unilinde nafsi yangu na kuniponya,Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe.