1. Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu,
2. Ee Mungu wangu,Nimekutumaini Wewe, nisiaibike,Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.
3. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja;Wataaibika watendao uhaini bila sababu.
4. Ee BWANA, unijulishe njia zako,Unifundishe mapito yako,
5. Uniongoze katika kweli yako,Na kunifundisha.Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu,Nakungoja Wewe mchana kutwa.
6. Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako,Maana zimekuwako tokea zamani.