9. Aliziinamisha mbingu akashuka,Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.
10. Akapanda juu ya kerubi akaruka,Naam, aliruka upesi juu ya mabawa ya upepo.
11. Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha,Kuwa hema yake ya kumzunguka.Giza la maji na mawingu makuu ya mbinguni.
12. Toka mwangaza uliokuwa mbele zakeKukapita mawingu yake makuu.Mvua ya mawe na makaa ya moto.
13. BWANA alipiga radi mbinguni,Yeye Aliye juu akaitoa sauti yake,Mvua ya mawe na makaa ya moto.
14. Akaipiga mishale yake akawatawanya,Naam, umeme mwingi sana, akawatapanya.
15. Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji,Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa,Ee BWANA, kwa kukemea kwako,Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako.