Zab. 18:2-7 Swahili Union Version (SUV)

2. BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu,Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia,Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.

3. Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa,Hivyo nitaokoka na adui zangu.

4. Kamba za mauti zilinizunguka,Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.

5. Kamba za kuzimu zilinizunguka,Mitego ya mauti ikanikabili.

6. Katika shida yangu nalimwita BWANA,Na kumlalamikia Mungu wangu.Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,Kilio changu kikaingia masikioni mwake.

7. Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka,Misingi ya milima ikasuka-suka;Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu.

Zab. 18