Zab. 127:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. BWANA asipoijenga nyumbaWaijengao wafanya kazi bure.BWANA asipoulinda mjiYeye aulindaye akesha bure.

2. Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema,Na kukawia kwenda kulala,Na kula chakula cha taabu;Yeye humpa mpenzi wake usingizi.

3. Tazama, wana ndio urithi wa BWANA,Uzao wa tumbo ni thawabu.

4. Kama mishale mkononi mwa shujaa,Ndivyo walivyo wana wa ujanani.

Zab. 127