1. Haleluya.Heri mtu yule amchaye BWANA,Apendezwaye sana na maagizo yake.
2. Wazao wake watakuwa hodari duniani;Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
3. Nyumbani mwake mna utajiri na mali,Na haki yake yakaa milele.
4. Nuru huwazukia wenye adili gizani;Ana fadhili na huruma na haki.
5. Heri atendaye fadhili na kukopesha;Atengenezaye mambo yake kwa haki.
6. Kwa maana hataondoshwa kamwe;Mwenye haki atakumbukwa milele.
7. Hataogopa habari mbaya;Moyo wake u imara ukimtumaini BWANA.
8. Moyo wake umethibitika hataogopa,Hata awaone watesi wake wameshindwa.